Sitaki mchezo: Zari amjia juu Diamond


Mwanamuziki wa Bongo fleva Naseeb Abdul ajulikanaye kama Diamond Platinumz ameingia katika misukosuko na familia yake Baada ya kutangaza hadharani kuwa mtoto wa mwanamitindi Hamisa Mobeto ni damu yake na walikubaliana yeye na Mobeto kumlea mtoto huyo.
Maji yalizidi unga pale Diamond aliposema kwamba alishakaa chini na mpenzi wake Zari na kuelewana kuhusu ishu hiyo.
Wakati mahojiano hayo yakiendelea, Zari alikuja mbogo na kumchana live mpenzi wake huyo.
Katika mtandao wa snapshot Zari aliandika:  "Hahahaha unajidanganya,unasema uongo kuhusu Mimi kujua michepuko yako .Malizana na balaa ulilolianzisha .Mimi kunyamaza haimaanishi ni mpumbavu. Kuwa makini na maneno yako.
Aliendelea:"Inawezekana Mimi ni mama watoto wako ndio maana nimekaa kimya.Labda ugoogle kuhusu defamation of character law suit,usinijaribu".
Hali hii imemuweka Diamond katika hali ya sintofahamu kuhusu sakata la familia yake.Alikuwa akihojiwa na kituo cha Clouds FM,Dares ala am.


Comments