Sasa ni vita: Asema waziri wa mambo ya nje wa Korea kaskazini

Korea Kaskazini imetishia kudungua ndege za Marekani katika anga ya kimataifa,wakidai kwamba ujumbe ulioandikwa na rais wa marekani Donald Trump kupitia mtandao wa Twitter wikiendi iliyopita uliashiria kuwa Marekani wametangaza Vita vya tatu vya dunia.
Waziri wa mambo ya Je wa Korea Kaskazini Ri Yong-ho amesema:" Dunia inapaswa kufahamu kuwa ni Marekani ndio ya kwanza kutangaza vita nchini mwetu." Alikusudia ujumbe wa Trump mtandaoni akisema utawala wa kidikteta wa Korea Kaskazini hautadumu kwa muda mrefu.
Katika hutuba yake ya kwanza kwa umoja wa mataifa jumanne iliyopita, Trump alionya kwamba endapo Marekani na nchi marafiki zitashambuliwa ,ataiangamiza Korea Kaskazini.

Ri aliongeza: “Kwa vile Marekani imetangaza Vita dhidi yetu, tuna kila sababu ya kuishambulia ipasavyo. Tutajua nani Kati yetu na wao atakayeangamia."
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa, António Guterres,ameonya kwamba majibizano hayo hayatasaidia kutatua mzozo huo utakaoathiri dunia nzima bali utazidi kufanya mambo kuwa magumu zaidi na akawataka viongozi wa pande zote mbili kulegeza misimamo yao.

Comments